Somo la Kushona eBook

Mhusika mkuu wa hadithi hii anafundishwa na mama yake kuhusu hali ya ulimwengu wetu wakati huu wa COVID-19. Mama yake pia anamfundisha kushona barakoa ili aweze kuwasaidia wafanyakazi muhimu.

Available in these languages:

 

  • UKRAINIAN
  • HEBREW
  • GREEK
  • ROMANIAN

$9.99

500 in stock

Description

Taa na kelele za ajabu kutoka sebuleni zinamuamsha mhusika mkuu wa hadithi hii. Kuelewa kile kinachoendelea, anaenda chumbani ambapo mama yake alipo, na anamuona mama yake akishona barakoa za kinga. Mama yake anamwambia kwamba kutoka sasa wafanyakazi muhimu wote na wale wote wanaohitaji kusafiri kwenda kazini watahitaji kuvaa barakoa. Anapo tafakari maneno ya mama yake, anaamua ya kwamba yeye pia atavaa barakoa ya rangi nyingi ilioshonwa na mama yake, na anamwomba mama yake amfundishe jinsi ya kushona. Anataka kumshonea babu yake barakoa, na babu yake, akiwa amejazwa na furaha kwa sababu ya kitendo cha fadhili cha mjukuu wake, anamkumbatia alipotoka kazini hospitalini.
 

About the Author

Deana Sobel Lederman ni mwandishi na mchoraji. Bibi yake alikuwa mchoraji ambaye alisomea kwenye chuo kiitwacho
The Art Students League of New York. Alimfundisha Deana kuhusu uchoraji wakati Deana alikuwa mchanga sana, na mamake Deana pia alimhimiza kuchora kutoka wakati Deana alikuwa mchanga. Deana alichora kitabu chake cha kwanza cha ucheshi kinachoitwa The Wacky Couples wakati alikuwa na miaka minane, na baadaye alikuwa mchoraji mkuu wa gazeti la wanafunzi wa UC Berkeley na msanii aliyechapishwa. Baadaye, alisomea kuhusu sheria ya hakimiliki kwenye chuo kikuu cha sheria. Ameishi New York City; Berkeley, California; London, England; na Cambridge, Massachusetts. Deana alikulia katika mji wa San Diego, California, na hapo ndipo anapoishi pamoja na mume wake na watoto wake wawili.

Additional information

To Be Read Books

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Somo la Kushona eBook”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.