Description
Wahusika wachanga wa hadithi hii wameambiwa na familia zao kwamba kutoka sasa watu wote watahitaji kuvaa barakoa za kinga na watahitaji kukaa mbali mmoja kwa mwingine.
Wakiwa na barakoa mpya kwenye nyuso zao, hawo vijana wanaamua kwenda kwenye duka la aiskrimu na wazazi wao. Wanaona ni mzaha watu wazima mitaani wakivalia kofia za ajabu kama ukumbusho wa hizo sheria mpya. Kwa hali yoyote, ile utumizi wa barakoa na kutotangamana na watu haziwafadhaishi, na furaha yao inazidi wanapoonana kwenye foleni ya duka la aiskrimu. Wakati kila mmoja wao ameingia dukani kwa zamu yake na amenunua aiskrimu, wote wanarudi nyumbani kufurahia peremende zao.
Deana Sobel Lederman ni mwandishi na mchoraji. Bibi yake alikuwa mchoraji ambaye alisomea kwenye chuo kiitwacho
The Art Students League of New York. Alimfundisha Deana kuhusu uchoraji wakati Deana alikuwa mchanga sana, na mamake Deana pia alimhimiza kuchora kutoka wakati Deana alikuwa mchanga. Deana alichora kitabu chake cha kwanza cha ucheshi kinachoitwa The Wacky Couples wakati alikuwa na miaka minane, na baadaye alikuwa mchoraji mkuu wa gazeti la wanafunzi wa UC Berkeley na msanii aliyechapishwa. Baadaye, alisomea kuhusu sheria ya hakimiliki kwenye chuo kikuu cha sheria. Ameishi New York City; Berkeley, California; London, England; na Cambridge, Massachusetts. Deana alikulia katika mji wa San Diego, California, na hapo ndipo anapoishi pamoja na mume wake na watoto wake wawili.
Reviews
There are no reviews yet.